Ads 468x60px

Jumamosi, 10 Desemba 2016

MGANGA WA MASTAA BONGO AKIWEMO DIAMOND ANASWA LIVE..


Waandishi wetu


Laivu! Ile Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers imemfungia kazi na kumnasa sangoma anayedaiwa kuwafanyia mastaa mandigo akiwemo Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ili wang’ae kwa kuwasafishia nyota aitwaye Khalid Tege.


Sangoma anayedaiwa kuwafanyia mastaa mandigo akiwemo Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ili wang’ae kwa kuwasafishia nyota aitwaye Khalid Tege. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, jamaa huyo amekuwa akifuatwa na mastaa kibao wa Bongo kwenye ofisi yake iliyopo Magomeni-Kagera jijini Dar ili awafanyie

dawa.Baada ya kuzinyaka taarifa hizo, OFM, kama kawaida yake ilizama mzigoni na kumtafuta mganga huyo kwa njia ya simu ambapo alikanusha vikali kujihusisha na shughuli za uganga na kudai yeye ni mfanyabiashara wa dawa za asili.

“Nani aliyekwambia mimi ni mganga? Hakuna kitu kama hicho, shughuli yangu kubwa ni kusambaza dawa za asili katika maduka mbalimbali Kariakoo na kama una picha zangu hata ukinitazama unadhani naweza nikafanana kuwa mganga ndugu yangu? Sijihusishi na hivyo vitu,” alisema mganga huyo.

Baada ya kukanusha kuwa hajihusishi na shughuli za uganga ndipo kamanda mmoja wa OFM mbali na yule aliyewasiliana naye akamtafuta kwa njia ya simu kwa lengo la kwenda kusafisha nyota na kumuelekeza ofisini kwake ambapo huwa anafanyia kazi maeneo ya Magomeni-Kagera.

Kikosi chetu hicho kilijipanga na kutinga eneo hilo kisha mtaalam huyo akamtuma kijana wake kwenda kuwapokea bila kujua kuwa ni OFM ambao waliamua kumfungia kazi baada ya kuchenga kufanya kazi za uganga.Khalid Tege akipozi. OFM ilipotinga ofisini kwake, mganga huyo aliwapokea kama wateja wengine na kuwahudumia.

Makamanda wawili wa OFM waliingia kwa gia ya kutaka kusafisha nyota huku mmojawapo akieleza shida yake kuwa anajihusisha na masuala ya sanaa hivyo anataka kung’aa awe msanii mkubwa kama walivyo mastaa wengine ambapo aliwatajia vifaa vilivyokuwa vinahitajika na gharama zake huku akiwa amepandisha maruhani.

Jamaa huyo aliwaambia OFM kuwa kusafisha nyota ili mambo yakae kwenye mstari gharama ni shilingi elfu thelathini (30,000) na kuwika kisanaa kama alivyo Diamond na wengine alimwambia atoe shilingi elfu hamsini na mbili (52,000) kwa ajili ya vifaa vya matibabu.

Pia mganga huyo aliwahitaji OFM kutoa fedha ya sadaka ya mizimu baada ya kupigiwa ramli na kutekeleza hilo huku wakiahidi kurudi siku nyingine
kutoa fedha hizo za kununulia vifaa na kupata tiba.

COMMENT HERE

SHARE