Ads 468x60px

Jumanne, 13 Desemba 2016

SIMBA SC Yachezea Vitasa vya Mtibwa SugarKLABU ya Simba ikiwa na kipa wake mpya Daniel Agyei, jana imekubali kichapo cha mabao 2-1 katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Simba ilikuwa na nafasi ya kusawazisha katika mechi hiyo lakini beki, Janvier Bokungu akakosa penalti. Kipigo cha Simba, kinapunguza makali ya watani wake Yanga ambao walichapwa kwa mabao 2-0 na JKU ya Zanzibar wikiendi iliyopita.

Kipigo cha Yanga kiliwaamsha Simba ambao walitumia muda mwingi kuwananga watani wao, lakini leo mambo yamegeuka. Unaweza kusema hakuna kuchekana kwa kuwa Yanga ndiyo wanaotamba sasa.

COMMENT HERE

SHARE