Ads 468x60px

Jumapili, 25 Juni 2017

Kichuya kaipa Stars ushindi wa kwanza COSAFA 2017


Magoli mawili ya Shiza Kichuya dakika ya 12 na 18 kipindi cha kwanza magoli amvayo yalidumu hadi mechi inamalizika nankuipa Stars ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Malawi.
Stars imeanza vyema mechi zake hatua ya makundi ambapo imepangwa Kundi A ikiwa na Malawi,

Mauritius na Angola. Kundi B kuna  timu za Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbamwe.
Baada ya mchezo huo, Kichuya ametangazwa Man of the Match baada ya kuonesha kiwango safi ikiwa ni pamoja na kufunga magoli mawili yaliyoisaidia Stars kupata pointi tatu.

Timu mbili (vinara wa kila kundi) watafuzu hatua ya robo fainali ambako watakuna na timu za Zambia, Botswana, Afrika Kusini, Namibia, Lesotho na Swaziland ambazo zenyewe zimepangwa kuanzia robo fainali zikisubiri washindi wa Kundi A na B kucheza robo fainali.

0 comments:

Chapisha Maoni

COMMENT HERE

SHARE