Ads 468x60px

Alhamisi, 19 Aprili 2018

Picha: Kinachojiri katika ukumbi wa harusi ya alikiba


 
Leo ndiyo siku ambayo msanii wa Bongo Fleva hapa nchini, Aly Kiba amefunga ndoa na mpenzi wake Aminah Rikesh ambaye ni raia wa Kenya, jijini Mombasa.


Ndoa hiyo ilifungwa asubuhi ya leo katika msikiti wa Ummul Kulthum uliopo Mombasa na sherehe ya harusi inatarajiwa kufanyika hapo baadae katika ukumbi wa Diamond Jubilee ulioko jijini humo.

Harusi hiyo imetajwa kuwa ni ya gharama kubwa kutokana na bwana harusi mwenyewe kuwa ni mtu maarufu na itahudhuriwa na watu mbalimbali maarufu.


Harusi hiyo itarushwa mubashara na kituo cha runinga cha Azam hapo jioni.


Hizi hapa ni baadhi ya picha ya kinachoendelea katika ukumbi huo, ambapo sherehe ya harusi itafanyika.
0 comments:

Chapisha Maoni

COMMENT HERE

SHARE